NEWS

Friday 27 September 2019

WATU WENYE UALBINO WAJA NA MPANGO WA KUKUZA KIPATO NA UTALII WA NDANI + VIDEO




Chama cha watu wenye uwalibino   kimepanga kuzindua programu maalumu ambayo inalenga kukuza kipato cha watu wenye ualibino na utalii wa ndani.

 Uzinduzi wa programu hiyo inayofahamika kama Albinism Sports & Culture Tour utafanyika  Jumapili ya Septemba 29, katika viwanja vya Serengeti Mjini Tarime .

Katibu wa Mkuu wa Albinism Sports Club  Joseph Sinda  amesema  timu za mpira wa miguu  za watu wenye ualbino kutoka DR Congo na Kenya  zitashiriki katika uzinduzi wa programu hiyo .

  Lengo la programu hii ni kuongeza uelewa juu ya ualbino lakini pia kuhamasisha jamii kuweza kutushirikisha katika shughuli za kiuchumi, kijamii na kisiasa . Tutafanya hayo kapitia michezo na sanaa ambazo zinafanywa na watu wenye ualbino”, Sinda  aliwaambia waandishi wa habari mjini Tarime jana.

Sinda alisema programu hiyo itahusisha uendeshaji wa harambee  mbalimbali kuchangisha  fedha kwa ajili ya kuanzisha miradi ya kiuchumi  ambayo itasadia  kuhudumia  watu wenye ualbino .

 Mfano Sinda ambaye pia ni mwenyekiti wa watu wenye ualbino Wilaya ya Tarime alisema wana mpango wa kuanzia kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti.

Aidha Sinda amesema  programu hiyo  itasadia kukuza utalii wa ndani .

“ Progamu hii itazinduliwa Tarime na mara baada ya uzinduzi tutatembelea  mbuga mbalimbali . Tutaanza kutembelea hifadhi ya taifa ya Serengeti kwa uwezesho wa shirika la hifadhi za taifa (TANAPA)”, alisema Sinda.

TAZAMA VIDEO :

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages