NEWS

Saturday 28 September 2019

NAMBA TATU AZUNGUMZA NA WAHITIMU CHUO CHA AFYA SHIRATI
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Samweli Kiboye Namba Tatu ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa huo  kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.

 Namba Tatu ametoa wito huo jana Ijumaa Septemba 27,2019 katika mahafali ya 57 ya wahitimu kozi ya uuguzi stashahada na cheti,pamoja na wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika chuo cha cha Sayansi za Afya Shirati kilichopo Wilayani Rorya. 

Mwenyekiti huyo wa CCM  pia alitawaka wahitimu hao kutumia vyema taaluma kutoa huduma bora kwa  wananchi. 

Awali Mkuu wa chuo hicho  Beatrice Mungure aalisema chuo hicho kina mpango wa kuanzisha kozi ya   wataalamu wa maabara,kusomesha walimu ngazi ya shahada ya kwanza,na kuongeza majengo muhimu ya watumishi,na ukumbi wa mikutano.
Kwa upande wao wahitimu wa Chuo Cha Sayansi za Afya Shirati walisema wako tayari kutoa huduma bora za Afya kwa jamii bila kusahau kujiendeleza.


Chuo Cha Sayansi za Afya Shirati kilijengwa mwaka 1959 na kuanza kutoa  mafunzo ya uuguzi ngazi ya cheti  mwaka 1960 kikiwa na wanachuo 13.
Hivi sasa chuo hicho kina uwezo wa kuchukua zaidi ya wanachuo 250, kwa mujibu wa taarifa ya mkuu wa chuo.

TAZAMA VIDEO 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages