Mwanafunzi wa kwanza katika matokeo ya darasa la saba mwaka
2019 ni Grace Imori Manga kutoka shule ya
Msingi Graiyaki iliyopo Wilayani Serengeti Mkoa wa Mara.
Matokeo hayo yametangazwa
leo na Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani
Tanzania (NECTA) Dkt Charles Msonde .
Dkt Msonde amemtangaza Grace kuwa ndiye mwanafunzi bora kitaifa.
Aidha shule hiyo ya msingi ya Graiyaki imeshika nafasi ya kwanza katika shule 10 bora
kitaifa ikifutia na shule ya Twibhoki ambayo pia ipo Mkoani Mara .
No comments:
Post a Comment