NEWS

Tuesday 26 November 2019

AYE YAANDAA MBIO ZA MARATHON BUNDATaasisi ya African Youth Empowerment (AYE) Kanda ya Ziwa imeandaa mbio za Marathon ambazo zitafanyika  Mjini Bunda Mkoani Mara Disemba 12 mwaka huu ambapo mshindi wa wakwanza atazawadiwa  shilingi laki mbili.
Mratibu wa AYE Kanda ya Ziwa Hussein Musa ameiambia  Mara Online News kuwa mbio hizo zitahusisha watoto kuanzia umri wa miaka 10-15, wazee, watumishi wa serikali na washiriki rasmi wa mbio hizo.
  Maandalizi ya mbio hizo yanaendelea vizuri na usajili umeshaanza”, amesema mratibu  wa AYE Kanda ya ZIWA.
AYE ni taasisi ambayo inasadia kuendeleza maisha ya vijana kielimu, kiuchimi na kimichezo .

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages