KLABU
ya Waandishi wa Habari Kanda ya Kati (CPC) imechagua viongozi wapya
watakaoitumikia kwa kipindi cha miaka mitano.
Akitangaza
matokeo hayo jana Mei 2, 2020 jijini Dodoma, Mwenyekiti wa
uchaguzi huo, Abubakari Famau ambaye ni Mwakilishi wa Shirika la
Utangazaji Uingereza (BBC), amesema mshindi wa nafasi ya uenyekiti ni Mussa
Yusufu kutoka Uhuru Media.
Yusufu
amemtangaza mshindi wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Mbashiru Katare kutoka
Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).
Nafasi
ya Katibu Mkuu ilichukuliwa na Benchine Bango ambaye ni mwandishi huru, huku
Musa Enock kutoka AFM Radio akichaguliwa kuwa Msaidizi wake.
Waliochaguliwa
kuwa wajumbe wa Kamati Tendaji ya CPC ni Jasmine Shamwepu kutoka ABM Radio,
Doto Kwilasa kutoka Gazeti la Jamvi la Habari na Amani Mbando kutoka Channel
Ten.
(Habari na
Faustine Galafoni, Dodoma)
No comments:
Post a Comment