NEWS

Sunday 17 May 2020

WAZIRI MKUU AKAGUA MRADI WA KUZALISHA UMEME WA JNHPP

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Waziri wa Nishati Dkt. Medad Kalemani, wakati alipokagua hatua za utekelezaji wa mradi  wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha Megawati 2,115, May 14, 2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha Megawati 2,115 na amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Dkt. Tito Mwinuka asimamie mradi huo ili ukamilike kwa wakati.

Vilevile, Waziri Mkuu amemwagiza mkandarasi anayejenga mradi huo aukamilishe kwa wakati kwa sababu imebainika kuwa mvua zinazoendelea kunyesha nchini haziathiri utekelezaji wa ujenzi huo.
 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, (watatu kushoto) akikagua hatua za utekelezaji wa mradi  wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha Megawati 2,115, unaojengwa na kampuni ya Yapi Merkezi, May 14, 2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Alhamisi Mei 14, 2020) akiwa katika ziara ya kukagua hatua za utekelezaji wa mradi huo. Amesema ameridhishwa maedeleo ya ujenzi wa mradi huo mkubwa wa kimkakati.

“Nimetembelea eneo la mradi na kujionea shughuli zote zinazoendelea, kazi inayofanyika ni ya uhakika huku kukiwa na matumaini makubwa ya kukamilisha mradi mapema kabla ya muda uliopangwa.”
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Waziri wa Nishati Dkt. Medad Kalemani, wakati alipokagua hatua za utekelezaji wa mradi  wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha Megawati 2,115, May 14, 2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mradi wa umeme wa maporomoko ya maji ya Mto Rufiji unajengwa na kampuni ya Arab Construction kwa pamoja na kampuni ya Elsewedy Electric zote za kutoka nchini Misri. Mradi huo unatarajiwa kuzalisha Megawati 2,115 ambazo zitaingizwa kwenye grid ya Taifa na kuifanya nchi kuwa na umeme mwingi na wa uhakika.

Mbali na kuliwezesha Taifa kuwa na umeme wa uhakika, pia mradi huo umewezesha kupungua kwa changamoto ya ajira baada ya Watanzania wengi wakiwemo wakandarasi kupata ajira za kudumu na za muda mfupi.
 
Kukamilika kwa utekelezaji wa mradi huo, kutaiwezesha Tanzania kuzalisha kiasi kikubwa cha umeme kitakachosaidia kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa uchumi wa viwanda na mradi wa reli ya kisasa.
 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Serikali na kampuni ya Yapi Merkezi kabla ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi  wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), May 14, 2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Hafla ya utiaji saini ya Mkataba wa Ujenzi wa Mradi ilifanyika jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Desemba, 2018 na kushuhudiwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wa Misri Dkt. Mostafa Madbouly. Mradi huu ni njia sahihi ya kufikia Uchumi wa Viwanda ifikapo mwaka 2025
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, (watatu kushoto) akikagua hatua za utekelezaji wa mradi  wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha Megawati 2,115, unaojengwa na kampuni ya Yapi Merkezi, May 14, 2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages