NEWS

Monday 1 June 2020

Mwenyekiti wa Chadema atimkia CCM Bariadi


CHADEMA kimeendelea kumeguka baada ya Mwenyekiti wake Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Lazaro Singibala na wanachama wanne kukihama na kujiunga CCM.
Mwenyekiti wa Chadema aliyehamia CCM, Lazaro Singibala (mwenye kofia ya kijani)

Simngibala na wenzake wamepokewa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bariadi, Juliana Mahongo leo Juni 1, 2020 katika ofisi za chama hicho mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bariadi, Juliana Mahongo


Katika mapokezi hayo alikuwepo Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga ambaye amewahakikishia wanachama hao wapya kuwa wamehamia kwenye chama sahihi na salama.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga 
Mara baada ya kupokewa, Singibala amesema ameamua kuhamia CCM baada ya kuridhishwa na kazi nzuri zinazofanywa na Rais Dkt John Magufuli katika kuwaletea Watanzania maendeleo.
Baadhi ya wanachama wa CCM) Wilaya ya Bariadi
Mmoja wa wanachama wa Chadema waliofuatana na Singibala kuhamia CCM, David Benjamin, ameahidi kwamba watakuwa wanachama waaminifu na wako tayari kukitumikia chama hicho tawala.(Imeandikwa na Anita Balingilaki, Bariadi)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages