Afisa Elimu Mkoa wa Mara Ephraim Simbeye (Watatu kulia) akitoa maelekezo kwa wanafunzi wa kidato cha sita jinsi ya kuchukua tahadhari dhidi ya Corona na kusoma kwa bidii |
Mkuu wa shule ya Sekondari Tarime Machota Kora akimpokea afisa elimu mkoa wa Mara Ephraim Simbeye alipotembelea shuleni hapo |
“Walimu tufanyeni kazi kwa kujituma niliwahi kusoma mahala fulani
kuwa ualimu ni wito hivyo wito huo uonekane katika ufaulu hatutaki alama
‘zero’alisisitiza REO Simbeye.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha sita wakinawa mikono kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona |
Kwa
upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari
Tarime, Machota Kora amemhakikishia REO huyo kuwa wameandaa utaratibu mzuri
kuwanoa wanafunzi hao ili waweze kufanya vizuri katika mtihani wao.
“
Tayari tumemaliza mada zote hivyo
tunachofanya kwa sasa ni kufanya marudio na nitahakikisha nakuwepo pamoja na
walimu wangu wakati wa muda wa usiku wa kujisomea kwa wanafunzi hao ili
kuhakikisha tunatoa msaada pale wanafunzi hao watakapokwama’’ alisema Machota.
Wanafunzi wa kidato cha sita wakiwa paredi |
(Habari na Clonel Mwegendao, Tarime)
No comments:
Post a Comment