NEWS

Wednesday 8 July 2020

Jafari Chege awania ubunge Rorya kuwapaisha wananchi kiuchumi


KADA kijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jafari W. Chege, ametangaza nia ya kugombea ubunge Rorya kwa dhamira ya kujenga mfumo wa kuinua kipato cha kila mkazi wa jimbo hilo kupitia sekta mbalimbali.
 Chege, kijana msomi mwenye digrii ya uwekezaji kwenye miliki na fedha, ametangaza nia hiyo leo Julai 8, 2020 katika mazungumzo maalumu na Mara Online News akisema yeye kama Mwanarorya ameguswa na hali duni ya kiuchumi inayoendelea kuwatesa Wanarorya wengi, hivyo ameamua kuomba ubunge ili atumie nafasi hiyo kufungua milango ya maendeleo ya kweli yatakayomgusa kila mwananchi jimboni humo.

Chege ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Nyihara katika kata ya Kyang’ombe wilayani Rorya, amesema akifanikiwa kuteuliwa na CCM na baadaye kupata ridhaa ya wananchi ya kuwa mbunge wa Rorya, ataelekeza nguvu kubwa katika kuhakikisha Wanarorya wananufaika ipasavyo na shughuli za kilimo, uvuvi na mifugo, lakini pia kuwaondolea adha katika huduma za maji, afya na elimu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages