NEWS

Tuesday 7 July 2020

Tarime Mji yapokea bilioni 2 kuboresha miradi ya kijamii
HALMASHAURI ya Mji wa Tarime mkoani Mara imepokea shilingi zaidi ya bilioni mbili kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya kugharimia ujenzi na ukarabati wa miundombinu mbalimbali ya taasisi za kijamii.
 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Elias Ntiruhungwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake.


Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Elias Ntiruhungwa, amewaambia waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumanne Julai 7, 2020 kwamba wamepokea fedha hizo hivi karibuni na tayari baadhi zimeanza kutumika kama ilivyokusudiwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Ntiruhungwa na timu yake wakikagua vibanda vya biashara katika soko la Rebu, ambalo pia litanufaika na sehemu ya shilingi bilioni mbili zilizotolewa na Serikali Kuu.
Ntiruhungwa ametaja baadhi ya taasisi zitakazonufaika na kiasi cha fedha kikiwa kwenye mabano kuwa ni Shule ya Sekondari ya Tarime (milioni 968.7) na Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime (milioni 400).

Amefafanua kuwa fedha hizo zitatumika kugharimia ujenzi na ukarabati wa miundombinu mbalimbali ikiwemo vyumba vya madarasa, nyumba za watumishi na mifumo ya maji na umeme katika taasisi hizo.

(Imeandikwa na Mara Online News)


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages