Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Elias
Ntiruhungwa akiongea na wakuu wa idara pamoja na wawezeshaji katika mafunzo ya uhakiki wa kaya maskini yaliyoandaliwa na TASAF
|
Mafunzo
hayo ya siku mbili ambayo pia yamehusisha wakuu wa idara wa Halmshauri
hiyo yatafuatiwa na kazi ya uhakiki wa kaya za walengwa kwa lengo la
kuondoa wanufaika hewa.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Elias Ntiruhungwa, amewataka washiriki
wa mafunzo hayo kufanikisha kazi hiyo inayotarajiwa kufanyika kote
nchini.
Kwa upande wake, Nisalile Brown Mwaipasi(anayeongea pichani) kutoka TASAF, amesema kazi ya uhakiki inalenga kusafisha daftari la walengwa.
Mwaipasi
amesema takwimu zinaonesha kuwa utekelezaji wa mpango huo kwa kipindi
cha kwanza umechangia kupunguza umaskini wa mahitaji ya msingi kwa kaya
kwa asilimia 10 na umaskini uliokithiri umepungua kwa asilimia 12 kwa
kaya maskini sana nchini.
Wakuu wa idara na wawezeshaji wa TASAF katika Halmashauri ya Mji wa Tarime wakiwa kwenye mafunzo leo |
(Imeandikwa na Mara Online News, Tarime
No comments:
Post a Comment