NEWS

Friday, 16 January 2026

Kiles atuma salamu za pole kifo cha kada wa CCM kijana Macheda



Simion Samwel Kiles "K"

Na Mwandishi Wetu
Tarime
-----------

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini), Simion Samwel Kiles (K), ametuma salamu za pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na wana-Tarime kwa ujumla kufuatia kifo cha kijana Wambura Kisike maarufu kwa jina la Macheda.

Akizungumza na Mara Online News mjini Tarime leo, Kiles ambaye pia alikuwa Diwani wa Kata ya Nyakonga kwa tiketi ya CCM, ameeleza kusikitishwa na taarifa za kifo cha kijana huyo.

Macheda ambaye alikuwa fundi umeme na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), inadaiwa alijinyonga kwa shuka chumbani kwake katika mtaa wa Nkende mjini Tarime, ambapo taarifa za kifo chake zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii jana mchana.


Macheda enzi za uhai

Mwili wa Macheda umesafirishwa leo kwenda nyumbani kwao jijini Mwanza kwa ajili ya mazishi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages