NEWS

Monday 31 August 2020

Kembaki aahidi maji safi Tarime Mjini, Waitara aonya wapinzani

Mgombea ubunge jimbo la Tarime Mjini, Michael Kembaki (CCM) akihutubia mkutano mkubwa wa wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni zake mjini Tarime, jana.

MGOMBE ubunge jimbo la Tarime Mjini kwa tiketi ya CCM, Michael Kembaki, amesema tatizo la ukosefu wa maji safi ya bomba katika mji wa Tarime na viunga vyake ni miongoni mwa vipaumbele atakavyoshughulikia haraka baada ya kuchaguliwa.

 

Kembaki ametoa ahidi hiyo kwa umati mkubwa wa wakazi wa jimbo hilo alipowahutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni zake mjini Tarime, jana Agosti 30, 2020.

Wananchi wakimsikiliza mgombea ubunge jimbo la Tarime Mjini, Michael Kembaki (CCM) wakati wa uzinduzi wa kampeni zake mjini Tarime, jana.

 

Pia mgombea huyo ameahidi kwamba akichaguliwa kuwa mbunge atahakikisha kuwa ujenzi wa soko kuu la Tarime unaanza bila kuchelewa ili kuwapatia wananchi fursa ya kufanya biashara na kujiinua kiuchumi.

Mgombea ubunge jimbo la Tarime Mjini, Michael Kembaki (kulia) akisubiri kuhutubia mkutano wa uzinduzi wa kampeni zake mjini Tarime, jana. Kushoto ni mfanyabiashara maarufu wa wilayani Tarime, Peter Zakaria.


“Naombeni mnichague nitahakikisha mnapata maji safi na soko hili litajengwa,” amesema Kembaki na kuongeza “Ni aibu kwa mji wa Tarime kuendelea kuwa na shida ya maji.”

 

Akizungumza katika mkutano huo, mgombea ubunge jimbo la Tarime Vijijini pia kupitia CCM, Mwita Waitara, amewaomba wakazi wa Tarime kuchangua wagombea wanaotokana na chama hicho ili kupata maendeleo ya kisekta.

 

“Tuazime imani ya kura zenu tutawalipa maendeleo. Mtapata maendeleo ya elimu, barabara, umeme, maji ya tope itabaki historia hapa Tarime,” Waitara ameueleza umati wa wananchi hao.

Mgombea ubunge jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara (CCM) akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Tarime Mjini, Michael Kembaki mjini Tarime, jana.

 

Hata hivyo, Waitara ametumia nafasi hiyo pia kuonya kuwa CCM hakitavumilia kuona wanachama na wafuasi wake wakifanyiwa fujo na vyama vya upinzani katika majimbo yote mawili [Tarime Mjini na Tarime Vijijini] wakati wa kampeni.

 

“Hii ngoma ya mwaka huu sio ya mwaka 2015 na tumejipanga,” amesisitiza Waitara ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

 

Hata hivyo, Waitara amesema yeye na Kembaki watafanya kampeni za kistaarabu na staha. Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utafanyika nchini kote Oktoba 28, mwaka huu.

 

(Habari na picha zote na Mara Online News)

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages