NEWS

Monday 3 August 2020

TaCRI yapaa uzalishaji, usambazaji miche ya kahawa

TAASISI ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TaCRI) imeweka mkakati wa kuzalisha   na kusambaza kwa wakulima  miche ya kahawa milioni 23 kwa kushirikiana na Bodi ya Kahawa nchini (TCB) pamoja na wadau wengine  wanaoshiriki kutekeleza mkakati huo wa miaka mitatu.

   Hayo yamesemwa Agosti 3, 2020 na Mkuu wa Programu ya Usambazaji Technolojia na Mafunzo kutoka TacRI, Dkt Magesa Jeremiah, katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa wilayani Bariadi, Simiyu.

   Dkt Jeremiah ameongeza kuwa hadi June 30, 2020 wamezalisha na kusambaza miche 9,774,453 sawa na mafanikio kwa asilimia 98 ya makisio ya kuzalisha na kusambaza miche 9,991,383.

" Tumeendelea kutekeleza Mkakakati wa kuzalisha na kusambaza miche bora milioni 23 kwa kushirikiana na bodi ya kahawa", alisema Dkt Jeremiah.

   Amesema wameendelea kutoa maelekezo kwa wakulima 3,304, maafisa ugani 345, wakulima wahamasishaji 131, vikundi 257 vya wakulima na wadau wengine kuhusu namna bora ya utunzaji wa mibuni kutokea shambani, usindikaji, ukaushaji na ubora mpaka wakati wa kuuza kahawa.

Mkuu was Programu ya Usambazaji Technolojia na Mafunzo kutoka TaCRI, Dkt Magesa Jeremiah kwenye banda la maonesho

Ameongeza kuwa wameboresha usimamizi na uendeshaji wa vitalu vya miche bora kwenye vikundi, mashamba makubwa ya kahawa ya wakulima binafsi, kuanzisha mashamba darasa 102, kusambaza vipeperueshi 5,340 na kufanya ziara za kutoa ushauri wa kitaalamu kwenye halmashauri 69 katika mikoa 18 ndani ya kanda sita zinazolima kahawa nchini.

   Dkt Jeremiah amesema kwamba kwa mwaka ujao wa fedha 2020/21 pamoja na kazi nyingine za kusambaza technolojia, malengo yao ni kuzalisha miche milioni 15.

  

Hata hivyo, Dkt Jeremiah ametaja baadhi ya changamoto zinazoikabili TaCRI kuwa ni bei kubwa ya pembejeo za kilimo cha kahawa ikiwa ni pamoha na VAT ambayo amesema ingeweza kupunguzwa au kuondolewa kabisa, uhitaji mkubwa wa miche  bora ya kahawa kwa kipindi kifupi kutokana na wadau wengi kuhamasika na kutambua umuhimu wa aina bora za mbegu, uhaba wa maji kwenye bustani za miche ya kahawa na maji safi kwa ajili ya usindikaji wa kahawa bora.

 (Imeandikwa na Anita Balingilaki, Bariadi) 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages