NEWS

Sunday, 20 September 2020

Majaliwa: Nileteeni Kembaki bungeni tuharakishe maendeleo Tarime Mjini

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kushoto) akimnadi mgombea ubunge jimbo la Tarime Mjini kwa tiketi ya CCM, Michael Kembaki katika mkutano wa kampeni kwenye viwanja vya soko la zamani la Tarime.

 

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CCM, Kassim Majaliwa amewaomba wakazii wa jimbo la Tarime Mjini kumchagua mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya chama hicho, Michael Kembaki ili waweze kupata maendeleo ya haraka. 

 

“Mlete Kembaki bungeni, mchagueni Kembaki tulete maendeleo,” Majaliwa amesisitiza leo Septemba 20, 2020 wakati akihutubia mkutano wa kampeni katika viwanja vya soko la zamani mjini Tarime. 

Mgombea ubunge jimbo la Tarime Mjini kwa tiketi ya CCM, Michael Kembaki (kulia juu) akiwanadi wagombea udiwani (waliosimama mbele) katika kata mbalimbali kupitia chama hicho wakati wa mkutano wa kampeni uliohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye viwanja vya soko la zamani la Tarime leo.

 

Majaliwa amesema Kembaki akichaguliwa moja ya kazi yake kwanza ni kuhakikisha kuwa ujenzi wa soko la Tarime mjini unafanyika bila kuchelewa. 

 

Amesisitiza umuhimu wa kuchagua viongozi wa CCM akisema chama hicho tawala ni benki ya viongozi waadilifu na wachapa kazi. 

Wananchi wakishangilia katika mkutano wa kampeni uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye viwanja vya soko la zamani la Tarime leo, ambapo amewaombea kura mgombea ubunge jimbo la Tarime Mjiji kupitia CCM, Michael Kembaki na madiwani wanaotokana na chama hicho jimboni humo.

 

“Chagua kwa mtiririko mzuri. Chagua mafiga matatu [rais, mbunge na diwani wa CCM] ambayo yanaweza kuivisha chakula vizuri,” amesema Majaliwa. 

 

Waziri Mkuu huyo ameongeza “CCM ni benki ya viongozi wenye uadhilifu na uwezo wa kuongoza.” 

 

Aidha, amewahakikishia wananchi kuwa mji wa Tarime upo kwenye orodha ya miji 28 ambayo itanufaika na mradi mkuwa wa maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria takaomaliza tatizo la maji katika mji huo.

 

(Habari na picha zote na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages