NEWS

Thursday 17 September 2020

Ndaki aahidi makubwa Maswa Magharibi

Mgombea ubunge Maswa Magharibi, Mashimba Ndaki (CCM), akijinadi kwa wananchi wa jimbo hilo wakati wa uzinduzi wa kampeni zake, juzi.


MGOMBEA ubunge Maswa Magharibi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mashimba Ndaki, amesema akichaguliwa atashirikiana na serikali kusukuma utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwamo ya maji ili ikamilike kwa wakati na kuanza kuwasaidia wananchi jimboni humo.

 

Ndaki ametoa ahadi hiyo kwa wakazi wa jimbo hilo wakati wa uzinduzi wa kampeni zake juzi, ambapo pia amesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita miradi mingi ikiwemo ya maji imekamilika katika kata nyingi na mingine iko kwenye hatua nzuri.

Sehemu ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza mgombea ubunge jimbo la Maswa Magharibi, Mashamba Ndaki (CCM), juzi.

 

Pia ameahidi kuanzisha Saccos za wanawake na vijana na kwamba kwa kuanzia atazichangia Sh milioni kumi kila moja ili kuziwezesha kukopa na kukuza mitaji.

 

“Tutatengeneza uongozi ambao utahakikisha fedha hiyo inakuwa salama na mtakuwa mnakopeshana na hii itaanza mwanzoni mwa Desemba 2020, tutakuwa na vijana Saccos Maswa Magharibi na wanawake nao watakuwa na Saccos yao, kila Saccos nitatoa milioni kumi," amesisitiza Ndaki.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Maswa, Mhandisi Paul Jidayi (kushoto) akimnadi kwa wananchi mgombea ubunge jimbo la Maswa Magharibi, Mashamba Ndaki (kulia), juzi.


Awali, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Maswa, Mhandisi Paul Jidayi, amewaomba wananchi kuwachagua wagombea wanaotokana na chama hicho kwa nafasi za urais, ubunge na udiwani.

Baadhi ya wagombea udiwani wa kata mbalimbali katika jimbo la Maswa Magharibi wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge, Mashamba Ndaki, juzi.

 

Aidha, Mhandisi Jidayi amewataka wagombea ubunge na udiwani wilayani hapo watakapochaguliwa kuhakikisha wanawatumikia wananchi kwa kiwango cha kuridhisha, huku akiwaomba wananchi nao kuhakikisha wanawachagua wagombea wote wanaotokana na chana hicho.

 

“T\unapiga kura kwa kuangalia ilani ya chama husika, wananchi tuichague CCM kwa maendeleo,” amesisitiza Mhandisi Jidayi.

 

(Habari na picha zote na Anita Balingilaki, Maswa)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages