NEWS

Thursday 17 September 2020

Waitara afunika ngome ya Heche Sirari

Mgombea ubunge Tarime Vijijini, Mwita Waitara (CCM), akihutubia wananchi katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni kata ya Sirari leo.

MGOMBEA ubunge jimbo la Tarime Vijijini kwa tiketi ya CCM, Mwita Waitara, leo Septemba 17, 2020 amepata mapokezi makubwa ya kikampeni katika mji mdogo wa Sirari anakotokea John Heche anayetetea kiti hicho kupitia Chadema.

 

Waitara alialikwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za mgombea udinwani kata ya Sirari, Amos Sagara (CCM), uliohudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi kwenye uwanja wa Tarafa.

Wananchi wakimsikiliza mgombea ubunge jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waiatara (hayupo pichani) katika mkutano wa uzinduzi wa kambeni kata ya Sirari leo.

 

Mbali ya kumnadi Sagara, Waitara na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Samwel Kiboye (Namba Tatu) wametumia mkutano huo kumwombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt John Magufuli na Waitara mwenyewe kwa nafasi ya jimbo la ubunge Tarime Vijijini.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Samwel Kiboye (kushoto) akiwanadi kwa wananchi wagombea Mwita Waiatara (katikati) na Amos Sagara (kulia) katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni kata ya Sirari uliofanyika kwenye uwanja wa Tarafa leo.

 

Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utafanyika nchini kote Oktoba 28, 2020.

 

(Habari na picha zote na Mara Online News) 

 

 


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages