NEWS

Monday 21 September 2020

Waitara azidi kujiimarisha kikampeni Tarime Vijijini

Mgombea ubunge jimbo la Tarime Vijijini kwa tiketi ya CCM, Mwita Waitara (katikati) akiwasili kijijini Kyoruba kwenye mkutano wake wa kampeni leo.


MGOMBEA ubunge Tarime Vijijini kwa tiketi ya CCM, Mwita Waitara leo Septemba 21, 2020 amewaomba wakazi wa kijiji cha Kyoruba jimboni humo kuchaguwa wagombea wanaotokana na chama hicho akiwemo yeye ili washirikiane katika kutatua changamoto zinazowakabili.

Mgombea ubunge jimbo la Tarime Vijijini kupitia CCM, Mwita Waitara akiomba kura kwa wananchi katika mkutano wake wa kampeni kijijini Kyoruba leo.

 

Waitara ameahidi kuwaboreshea wananchi hao huduma ya maji, kuwapelekea umeme na kuchangia gharama za ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho.

Wakazi wa kijiji cha Kyoruba wakiimba na kucheza kwa shangwe wakati wa kumpokea mgombea ubunge jimbo la Tarime Vijijini kwa tiketi ya CCM, Mwita Waitara alipokwenda kuwaomba kura leo.

 

Taarifa kutoka ndani ya CCM Wilaya ya Tarime zinasema mgombea huyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ameendelea kuimarisha kampeni zake jimboni humo.

Mkazi wa kijiji cha Kyoruba akisisitiza jambo katika mkutano wa kampeni wa mgombea ubunge wa jimbo la Tarime Vijijini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwita Waitara kijijini hapo leo.

 

Katika kinyang’anyiro cha ubunge Tarime Vijijini, Waitara anachuana na John Heche wa Chadema na Charles Mwera wa ACT - Wazalendo.

 

(Habari na picha zote na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages