NEWS

Sunday 18 October 2020

Waitara aahidi kijiji kipya Tarime Vijijini

Mgombea ubunge jimbo la Tarime Vijijini kwa tiketi ya CCM, Mwita Waitara akiwasili katika kijiji cha Kemakorere katani Nyarero kwa ajili ya mkutano wa kampeni, juzi.


MGOMBEA ubunge jimbo la Tarime Vijijini kwa tiketi ta CCM, Mwita Waitara amesema akifanikiwa kuchaguliwa atanzisha kijiji kipya kitakachoitwa Tais katika kata ya Bumera.

Waitara ametoa ahadi hiyo kujibu maombi ya wananchi wa eneo hilo katika mkutano wake wa kampeni katani humo, juzi.

Amesema kijiji kipya kitasadia kuharakisha huduma za kijamii kwa mamia ya wakazi wa eneo hilo.

Mamia ya wananchi wa kata ya Kemakorere wakimpokea kwa shangwe mgombea ubunge jimbo la Tarime Vijijini kupitia CCM, Mwita Waitara alipowasili kwa ajjili ya mkutano wake wa kampeni, juzi.


Baadaye Waitara amehutubia mkutano mkubwa wa wananchi katika kijiji cha Kemakorere, kata ya Nyarero ambako ameahidi kuhakikisha kinajengwa kituo cha afya na kuboresha huduma nyingine za jamii kama vile umeme kuwaka kila kitongoji.

Mamia ya wananchi wakimsikiliza na kumshangilia mgombea ubunge jimbo la Tarime Vijijini kwa tiketi ya CCM, Mwita Waitara (hayupo pichani) kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Kemakorere katani Nyarero, juzi. (Picha zote na Peter Hezron)

 

Mgombea huyo pia amewataka vijana kuepuka vitendo vya vurugu wakati wa uchaguzi na kukataa kutumiwa vibaya na wanasiasa.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages