Baadhi ya wakimbiaji wakishiriki mbio za Serengeti Safari Marathon ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti leo asubuhi. |
MASHINDANO ya mbio za Serengeti Safari Marathon yamefanyika kwa mvuto wa aina yake ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) eneo la Ndabaka Gate leo Novemba 14, 2020 kwa mbio za kilomita 5, 10, 21 na 42.
Sehemu nyingine ya wakimbiaji wakishiriki mbio za Serengeti Safari Marathon ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti leo asubuhi. |
Mashindando hayo yameshirikisha watalii kutoka mataifa mbalimbali, wanariadha kutoka mikoa ya Mara, Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Dar es Salaam, Arusha na Kilimanjaro, viongozi na watumishi wa Serikali, SENAPA na Shirika la Frankfurt Zoological Society (FZS).
Baadhi ya viongozi walioshiriki mashindano hayo ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Regine Hess na Kamishna wa Uhifadhi TANAPA ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt Allan Kijazi,
Viongozi wengine ni Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Caroline Mthapula, Msimamizi wa miradi ya wafadhili FZS, Michael Thompson, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Kanda ya Magharibi, Martin Loiboki na Mhifadhi Mkuu wa SENAPA, Masana Mwishawa, Meneja Mradi FZS Serengeti, Masegeri Rurai.
Mwishawa amesema mashindano hayo ya Serengeti Safari Marathon yamewashirikisha wakimbiaji zaidi ya 1,000, wengi wao wakiwa vijana wa jinsia zote.
Mgeni rasmi wa mashindano hayo ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Tanzania, Jakaya Kikwete.
(Imeandikwa na Mara Online News)
No comments:
Post a Comment