NEWS

Monday 2 November 2020

RPC Mkonda awahakikishia wananchi Tarime-Rorya usalama, amani

ACP William Mkonda

 

KAMANDA wa Polisi wa Mkoa (RPC) wa Kipolisi Tarime-Rorya, ACP William Mkonda, amewataka wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwa kuwa jeshi hilo limejipanga vyema kuhakikisha usalama, amani na utulivu vinaendelea kutamalaki mkoani humo.

 

ACP Mkonda ameyasema hayo leo Novemba 2, 2020 wakati akijibu swali la waandishi wa habari waliotaka kujua hali ya usalama katika mkoa huo baada ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliomalizika wiki iliyopita.

 

“Sisi kama jeshi la polisi tumejipanga vyema kuhakikisha hali hii ya utulivu na amani inaendelea - kwa kufanya doria za hapa na pale. Tunawahakikishia wananchi kwamba jeshi lao lipo kwa ajili yao kuhakikisha wanaendelea kuwa salama na kuhakikisha Mkoa wa Kipolisi Tarime-Rorya unaendelea kuwa na amani na utulivu,” amesisitiza Kamanda Mkonda.

 

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages