NEWS

Sunday 20 December 2020

'K' aahidi ujenzi makao makuu Tarime Vijijini, Waitara aonya ubadhirifu, Ghati aahidi ushirikiano

Kutoka Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Chomete, Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Vijijini, Simion K. Samwel, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mwita Waitara na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.

MWENYEKITI mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Vijijini, Simion K. Samwel amesema miongoni mwa vipaumbele vyaka ni kuhakikisha ujenzi wa makao makuu ya halmashauri hiyo unatekelezwa katika kipindi chake cha uongozi.

Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Vijijini, Simion K. Samwel akizungumza katika hafla hiyo.

Aidha, K amewataka madiwani wa halmashauri hiyo kufanyakazi kwa bindii ili kuendana na kazi ya Rais Dkt John Pombe Magufuli katika kuwaletea maendeleo wananchi.


K ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nyakonga, ameyasema hayo katika hafla ya pongezi na shukurani baada ya kuchaguliwa kuongoza halmashauri, ambayo imefanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya JK ya Nyamwaga, leo Desemba 20, 2020.

 

"Moja ya kipaumbele chetu ni kujenga makao makuu ya halmashauri," amesema K huku akiahidi kutoa ushirikiano kwa madiwani, watumishi wa serikali na wadau wote katika kupaisha maendeleo ya halmashauri hiyo.

 

Pia amehimiza umoja na mshikamano kama moja ya nguzo muhimu ya kuharakisha maendeleo ya halmashauri hiyo. "Umoja wetu ndio mafanikio yetu, hiki kiti nitakitendea haki, nanyi mtafurahi," amewahakikishia madiwani hao.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Chomete akizungumza katika hafla hiyo.

Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Chomete ameahidi ushirikiano kwa madiwani hao katika kushughulikia maendeleo ya wananchi.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mwita Waitara (kushoto) akipokewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Vijijini, Simion K. Samwel (katikati mwenye koti) na Mke wa K, Esther (kulia) kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya JK Nyamwaga.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mwita Waitara ambaye pia ni Mbunge wa Tarime Vijijini, amewataka madiwani kujiepusha na vitendo vya ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo ya wananchi katika kata zao.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mwita Waiatara akizungumza katika hafla hiyo.

"Ukila pesa za miradi ya maendeleo utafute mlango wa kutokea," Waitara ameonya, huku naye akiwataka madiwani kufuata nyayo za Rais Magufuli katika kuwatumikia wananchi.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime, Daudi Marwa Ngicho (kushoto) akiwatambulisha Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Chomete (katikati) na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mwita Waitara katika hafla hiyo.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tarime, Daudi Marwa Ngicho, amewataka madiwani wapya wa halmashauri hiyo kuhakikisha wanaacha alama ya maendeleo katatika kata zao ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuchaguliwa mwaka 2025.

 

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages