NEWS

Tuesday 22 December 2020

Mwenyekiti mpya Serengeti amulika kero ya vifusi Mugumu

Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Ayub Makuruma.

 

MWENYEKITI mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Ayub Makuruma, amekutana na wafanyabiasha wa mji wa Mugumu kusikiliza kero zao kwa ajili ya kuboresha mazingira ya biashara katika mji huo.

 

“Moja ya kero kubwa iliyoelezwa na wafanyabiashara wa Mugumu ni uwepo wa vifusi vilivyowekwa katika barabara za mitaa ya mji wa Mugumu tangu Machi mwaka huu,” Makuruma ameimbia Mara Online News, hivi karibunii.

 

Makuruma amesema utengenezaji wa barabara hizo ulipaswa kuwa umekamilika kufikia Oktoba mwaka huu, lakini vifusi vimeendelea kuwepo. “Vifusi vimekuwa kero na biashara nyingi zimesimama. Hii ni moja ya kero kubwa kwa wafanyabiashara katika mji wa Mugumu kwa sasa,” amesema.

Kikao cha kwanza cha Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Ayub Makuruma na wafanyabiashara wa mji wa Mugumu.

 

Baada ya kikao hicho, Makuruma amesema alifika ofisi za Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Serengeti na kuwasilisha kero hiyo.

 

“Nimeonana na Meneja wa TARURA amesema mvua ambazo zimekuwa zikinyesha zimekuwa ni moja ya sababu iliyochelewesha mradi huu,” amesema Makuruma ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Busawa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

 

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo wa Halmashauri amesema kero hiyo itafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.

 

Hivi karibuni, Makuruma ameweka historia kwa kuchaguliwa na madiwani wote 41 kuwa Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na kuahdi kuipasha halmashauri hiyo kimaendeleo.

 

“I want to see Serengeti on the sky and not on the ground,” amesisitiza Makuruma kwa lugha ya Kiingereza - akimaanisha “Nataka kuiona Serengeti ikipaa juu na sio ikishuka chini.”

 

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages