NEWS

Wednesday, 14 January 2026

Mara kupanda miti milioni 13 kwenye halmashauri zake zote



Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, akishiriki kampeni ya upandaji miti mjini Musoma leo.

Na Mwandishi Wetu
Musoma
--------------

Mkuu wa Mkoa (RC) wa Mara, Kanali Evans Mtambi, amesema wanatarajia kupanda miti milioni 13 katika halmashauri zote za mkoa huo, ikiwa ni mkakati wa utunzaji wa mazingira.

RC Mtambi ameyasema hayo leo Januari 14, 2026 mjini Musoma aliposhiriki upandaji miti kupitia Kampeni ya Mti wa Mama - maarufu kama 27 ya Kijani, inayoendeshwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).


Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Juma Chikoka, akipanda mti.

RC Mtambia amesema mkoa huo umeelekeza kila halmashauri kupanda miti milioni moja na nusu, ambapo kwa mwaka 2025 miti milioni saba ilipandwa.

Amesema Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti inafanya vizuri na kuongoza katika kupanda miti, kwani hadi ksasa tayari wamepanda miti milioni 1.2.

Kiongozi huyo amewataka wananchi wa mkoa huo kujenga mazoea ya kupanda miti katika maeneo yao badala ya kungoja maelekezo kutoka kwa wadau na serikali.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages