NEWS

Thursday 24 December 2020

Naibu Waziri Waitara awakumbuka wafungwa, mahabusu Tarime kwa ng’ombe, mchele wa Krismasi

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mwita Waitara (wa tatu kulia) akimkabidhi Mkuu wa Gereza la Tarime, Deusdedit Yamo (wa pili kulia) msaada wa ng'ombe atakayechinjwa kesho - Sikukuu ya Krismasi kwa ajili ya mlo wa wafungwa na mahabusu wa gereza hilo.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mwita Waitara (kushoto) akisaidiana na Mkuu wa Gereza la Tarime, Deusdedit Yamo kusogeza ng'ombe ambaye amemtoa msaada ili achinjwe kesho - Sikukuu ya Krismasi kwa ajili ya mlo wa wafungwa na mahabusu wa gereza hilo.

WAFUNGWA na mahabusu katika Gereza la Tarime mkoani Mara watasherehekea Sikukuu ya Krismasi kwa mlo mzuri baada ya Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mwita Waitara kuwapatia msaada wa ng’ombe mmoja, mchele kilo 100 na mafuta ya kula lita 20.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mwita Waitara (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Gereza la Tarime, Deusdedit Yamo msaada wa mchele na mafuta ya kula kwa ajili ya mlo wa wafungwa na mahabusu wa gereza hilo kesho - Sikukuu ya Krismasi.

Naibu Waziri Waitara ambaye pia ni Mbunge wa Tarime Vijijini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), amekabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Gereza la Tarime, Deusdedit Yamo gerezani hapo, leo Desemba 24, 2020.

 

Waitara amefuatana na viongozi mbalimbali wakati wa kukabidhi msaada huo - wakiwemo Katibu wa CCM, Hamis Kura, Diwani wa Kata ya Kenyamanyori, Farida Nchagwa na Diwani wa Viti Maalum, Nuru Hundi kutoka Halmashauri ya Mji wa Tarime.

 

“Niliahidi kuwapatia ndugu zetu wa gerezani msaada wa ng’ombe kwa ajili ya Sikukuu ya Krismasi, ninamshukuru Mungu leo nimeweza kutimiza ahadi hiyo,” amesema Naibu Waziri huyo anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mwita Waitara (wa pili kushoto) akizungumza na Mkuu wa Gereza la Tarime, Deusdedit Yamo (wa pili kulia) mara baada ya kumkabidhi msaada wa ng'ombe mmoja, mchele kilo 100 na mafuta ya kula lita 20 kwa ajili ya mlo wa wafungwa na mahabusu wa gereza hilo kesho - Sikukuu ya Krismasi. Wa kwanza kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime, Hamis Kura na Diwani wa Kata ya Kenyamanyori, Farida Nchagwa (kulia).
 

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Waitara amewataka wafungwa watakaofanikiwa kuachiwa huru kipindi hiki cha Sikukuu ya Kuzaliwa Yesu Kristo (Krismasi) kujitafakali na kuepuka kutenda makosa yanayoweza kuwarejesha gerezani.

 

Kwa upande wake, Mkuu wa Gereza hilo, Deusdedit Yamo, amemshukuru Naibu Waziri Waitara kwa kuwakumbuka wafungwa na mahabusu kwa msaada huo akisema utawawezesha kufurahia Sikukuu ya Krismasi.

Mkuu wa Gereza la Tarime, Deusdedit Yamo (katikati) akimpigia saluti ya salamu Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mwita Waitara (kulia) wakati alipowasili gerezani hapo kukabidhi msaada wa ng'ombe mmoja, mchele kilo 100 na mafuta ya kula lita 20 kwa ajili ya mlo wa wafungwa na mahabusu wa gereza hilo kesho - Sikukuu ya Krismasi.

 

Yamo ametumia nafasi hiyo pia kutoa wito kwa watu wengine wenye uwezo wa kiuchumi kuiga mgano huo wa Waitara kwa kujitokeza kuwapatia wafungwa na mahabusu wa gereza hilo misaada mbalimbali ya kibinadamu.

 

(Habari na picha zote na Mara Online News)

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages