NEWS

Thursday 24 December 2020

Mabilionea watano walioongeza utajiri wao zaidi 2020

 Hawa hapa ni mabilionea 5 walioongeza utajiri wao zaidi 2020

Mwaka 2020 ulikuwa mzuri sana kwa Elon Musk.

Tayari walikuwa mabilionea ... lakini utajiri wao uliongezeka zaidi mwaka 2020.

Bila shaka mwaka 2020 unaoelekea kumalizika ulikumbwa na changamoto nyingi kwa watu wengi, huku zaidi ya watu milioni 1.6 wakifariki dunia kutokana na janga la covid-19 duniani na mzozo wa kiuchumi uliosababisha biashara nyingi kufungwa na mamilioni ya ajira kupotezwa.

Hata hivyo watu tajiri zaidi duniani hawakuathiriwa na janga hilo.

Zaidi ya asilimia 60 ya mabilionea duniani waliongezea utajiri wao mwaka 2020 na watano wa kwanza ambao waliongezea utajiri wao kwa pamoja walikuza mali zao kwa dola bilioni 310.5.

Janga la corona liliathiri watu kwa njia tofauti

    1. Elon Musk, Mwanzilishi mwenza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Tesla

Elon Musk, mwanzilishi wa kampuni ya SpaceX na Afisa Mtendaji Mkuu wa Tesla, ameongeza takriban dola bilioni 140 ya biashara yake ya mwaka 2020.

Kutokana na hilo utajiri wake uliongezeka wa dola milioni 167,000 Jumatatu, kwa mujibu wa takwimu kutoka Bloomberg .

Hii ilitosha kumfanya Musk kupanda nafasi kadhaa katika orodha ya mabilionea na kumpita Bill Gates na kuchukua nafasi ya pili (baada ya Jeff Bezos) Novemba 2020.

Pia kulingana na jarida la Forbes ,hii ni mara ya kwanza katika mwaka bilionea kuongeza utajiri wake kwa kiwango hicho tangu jarida hilo lilipoanza kufuatilia mali ya mabilionea duniani.

    2. Jeff Bezos, mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Amazon

Jeff Bezos, ambaye pia ni mmiliki wa gazeti la Marekani la The Washington Post, alianza mwaka 2020 kama mtu tajiri zaidi duniani na kuumaliza akiwa vivyo hivyo.
Ongezeko la uuzaji mwaka 2020 limenufaisha Amazon, kampuni ya Jeff Bezos.


Alichofanya ni kuongeza zaidi ya dola 72 katika thamani yake, iliyochangiwa na ongezeko la mauzo ya mtandaoni katika kampuni yake Amazon kutokana na janga la corona.

Hapo hana mazoea ya kufanya shughuli za kutoa misaada, mwaka huu alijaribu kufanya hivyo:  Februari alitoa msaada wa dola bilioni 10 kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na Novemba alitoa karibu dola milioni 800 kusaidia mashirika ya mazingira.

Mtalaka wake, Mackenzie Scott alitoa msaada wa karibu dola bilioni 5.8 kwa mashirika ya misaada mwaka huo.

Mackenzie Scott ni mmoja wa wanawake tajiri duniani, hutoa karibu dola bilioni sita kutoka katika utajiri wake.

    3. Zhong Shanshan, mwanzilishi wa kampuni ya Nongfu Spring

Thamani ya utajiri wa Zhong Shanshan iliongezeka hadi dola za kimarekani bilion 62.6 (kwa sasa ni zaidi ya dola za kimarekani bilioni 69), kwa mujibu wa Bloomberg.
Zhong Shanshan kwa sasa ndiye mtu tajiri zaidi China

Zhong alikuwa mtu tajiri zaidi nchini China kufikia Septemba 2020 baada ya kampuni yake ya maji ya chupa, Nongfu Spring, kufanikiwa katika uuzaji wa hisa zake kwa umma na kupata dola bilioni 1.1 za Marekani.

Kampuni hiyo aliyoanzisha mwaka 1996 na inadhibiti asilimia tano ya soko ya la maji la Asia, ina thamani ya karibu Dola za Marekani milioni 70,000

Bilionea huyo mwenye umri wa miaka 66 pia anamiliki karibu asilimia 84 ya kampuni hiyo, utajiri unaokaridiwa kuwa karibu dola bilioni 60.

Hii ilimsaidia kuwapiku mabilionea wengine kama vile mwanzilishi wa Tencent Pony Ma na Alibaba, Jack Ma na kuwa mtu tajiri zaidi nchini China katika miezi ya hivi karibuni.

Zhong pia anasimamia kampuni ya utengenezaji chanjo ya Beijing Wantai Biological Pharmacy, ambayo iliuzwa kwa umma Aprili 2020.

Kampuni hiyo ilitengeneza chanjo ya Covid-19 ya kupuliza puani ambayo ilikuwa katika awamu ya pili ya majaribu Novemba 2020.

    4. Bernard Arnault, mmiliki wa maduka ya LVMH

Frenchman Bernard Arnault ndiye mtu tajiri zaidi katika nchi yake baada ya jarida la Forbes kumweka wa pili katika orodha ya watu tajiri zaidi, japo Bloomberg ilimuorothesha namba nne.
Licha ya kushuka kwa uuzaji wa bidhaa za kifahari, maduka ya LVMH yaliandikisha faida nzuri 2020


Mmiliki wa kampuni ya bidhaa za kifahari za LVMH, Arnault anakamilisha mwaka 2020 akiwa na utajiri wa thamani karibu dola bilioni 146.3.

Hata wakati ulimwengu ulikuwa unakabiliwa na janga la corona utajiri wa Arnault uliongezeka kwa zaidi ya asilimia 30 mwaka 2020.

Janga la corona lilipotokea LVMH iliacha kwa muda mpango wa kuinunua Tiffany & Co., lakini mwezi Oktoba ilifikia mkataba wa kuinunua kwa karibu dola bilioni 15.8, karibu dola za Marekani millioni 400 chini ya bei ya awali.

Uuzaji wa bidhaa za kifahari uliendelea kupungua, lakini LVMH iliwashangaza wawekezaji hivi karibuni ilipotangaza kuwa uuzaji wa mikoba ya Louis Vuitton na Dior ulisalia imara, hususan katika nchi kama Korea Kusini na China.

    5. Dan Gilbert, Rais wa kampuni za Rocket

Akiwa na umri wa miaka 58, Gilbert anamiliki timu ya mpira ya NBA Cleveland Cavaliers na mwanzilishi mwenza wa kampuni ya uuzaji nyumba kwa mkopo ya Quicken.


Kwa mujibu wa takwimu za Bloomberg, thamani yake iliongezeka kwa dola bilioni 28.1 mwaka 2020 (na kufikia dola za kimarekani 35.3), kutokana na kasi ya ukuaji ya kampuni mama ya Quicken Loans na Rocket.

Gilbert anamiliki asilimia 80 ya kampuni za Rocket, ambayo thamani yake inakadiriwa kuwa zaidi ya dola bilioni 31.

Utajiri wa Gilbert uliongezeka mwaka 2020 (mara sita zaidi kwa mwaka) kutokana na uuzaji wa hisa za Quicken kwa umma.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages