NEWS

Friday 22 January 2021

DC Tarime awatimua maofisa elimu kwenye kikao cha DCC

Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhandisi Mtemi Msafiri (katikati mbele) akizungumza katika kikao hicho. Kushoto ni Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara.

MKUU wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Mhandisi Mtemi Msafiri amewatimua maofisa elimu ya msingi na sekondari kutoka kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) baada ya kukosa takwimu za wanafunzi waliopata mimba.

 

Maofisa elimu hao wamekumbwa na tukio hilo leo Januari 22, 2021 katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu Tarime, baada ya Mhandisi Msafiri kuwataka watoe taarifa yenye takwimu hizo ambazo hawakuwa nazo kikaoni.

Washiriki wakifuatilia mada katika kikao hicho

Wakati huo huo, Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara ametangaza ‘ugomvi’ dhidi ya Ofisa Elimu Sekondari Wilaya ya Tarime kutokana na alichadai kuwa ameshindwa kusimamia elimu wilayani humo.

Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara (aliyesimama) akizungumza katika kikao hicho. Aliyekaa kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Apoo Castro Tindwa.

“Kwenye eneo hilo kuna shida, tutagombana sana maana ameshindwa kusimamia elimu, matokeo ya sekondari sio mazuri, ukimsikiliza afisa elimu mipango yake ni fake (haifai),” amesema Waitara ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Wadau kutoka taasisi mbalimbali zikiwamo benki za NMB na CRDB wakifuatilia mada katika kikao hicho.

Kikao hicho kimeongozwa na Mkuu wa Wilaya, Mhandisi Msafiri (Mwenyekiti) akisaidiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya, Apoo Castro Tindwa.

 

(Habari na picho zote na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages