NEWS

Tuesday 12 January 2021

Mbunge Ghati atimiza ahadi yake ujenzi wa madarasa Rorya

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Chomete.

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Chomete, ametimiza ahadi yake ya kutoa shilingi milioni moja kuchangia ununuzi wa mabati kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari wilayani Rorya.

 

Akizungumza na Mara Online News kwa njia ya simu leo Januari 13, 2021, Mbunge huyo amesema amewasilisha mchango wake huo mapema wiki hii.

 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Simon Odunga ameiambia Mara Online News kwa njia ya simu leo kwamba wadau mbalimbali wanaendelea kujitokeza kuchangia ujenzi huo.

 

“Michango inaendelea kutolewa, majengo yanaendelea kukamilishwa na baadhi yameshakamilika na kuanza kutumiwa na wanafunzi,” amesema Odunga.

Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Simon Odunga.

Michango hiyo imeitishwa na uongozi wa wilaya ya Rorya kwa ajili ya kugharimia ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuwezesha wanafunzi wote walioidhinishwa kuanza darasa la kwanza na kidato cha kwanza mwaka huu kupata nafasi ya kusomea.

 

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages