NEWS

Monday 25 January 2021

Mbunge Waitara amtumbua katibu wake

Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara.

MBUNGE wa Tarime Vijijini katika mkoa wa Mara, Mwita Waitara ametengua uteuzi wa Katibu wake kiofisi, Leonard Nyankang’a kuanzia leo Jumatatu Januari 25, 2021.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge Jimbo la Tarime Vijijini kwa umma leo, Waitara amemteua Remmy Mkapa kuchukua nafasi hiyo kuanzia leo.

Remmy Mkapa

 

Leonard Nyankang’a

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa Nyankang’a hatakiwi kujihusisha na shughuli zote za Ofisi ya Mbunge wa jimbo hilo kuanzia leo Januari 25, 2021.

 

Hata hivyo, taarifa hiyo haikueleza sababu ya kufanya mabadiliko hayo.

 

Waitara pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

 

#MaraOnlineNews - Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages