Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara (katikati) akisamilina na wananchi wa kata ya Kwihancha alipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara, jana Januari 8, 2021. |
MBUNGE wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara, jana Januari 8, 2021 amefanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Gibaso katani Kwihancha kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Katika hotuba yake, Waitara amewaambia mamia waliojitokeza kumsikiliza kwamba tayari amekwishatoa mabati 108 kwa ajili ya kuezeka vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Kwihancha.
Waitara akihutubia wananchi wa kata ya Kwihancha katika mkutano wa hadhara, jana. |
Kuhusu ukosefu wa vyoo vya walimu katika Shule ya Msingi Karakatonga, mbunge huyo amesema ameshawasilisha kero hiyo kwa Halmshauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini) kwa ajili ya utatuzi wa haraka.
Aidha, Waitara amesema halmashauri hiyo ina mpango wa kununua mtambo (katapila) kwa ajili ya ujenzi wa barabara zote jimboni humo.
“Katika bajeti ijayo halmashauri yetu imejipanga kununua grader kwa ajili ya ujenzi wa barabara na mtambo wa kuchimba visima vya maji katika maeneo yetu [Tarime vijijini],” amesema Waitara ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).
Mkazi wa kata ya Kwihancha akiwasilisha kero kwa Mbunge Waitara katika mkutano wa hadhara, jana. |
Changamoto nyingine zilizowasilishwana wananchi wa kata hiyo kwa mbunge huyo ni ukosefu wa umeme na mgogoro wa kugombea mpaka kati yao na maeneo ya uhifadhi wa wanyamapori, ambapo amesema anaendelea kuwasiliana na mamlaka husika kwa hatua za ufumbuzi.
(Habari na picha zote na Goefrey John wa Mara Online News)
No comments:
Post a Comment