NEWS

Saturday 9 January 2021

 Ndege ya shirika la ndege la Sriwijaya iliyokuwa imewabeba watu 62 imepoteza mawasiliano dakika chache baada ya kuruka kutoka mji mkuu wa Indonesia wa Jakarta.


Waziri wa usafirishaji wa Indonesia Budi Karya Sumadi, amesema ndege hiyo ilichelewa kuanza safari yake kwa muda wa saa moja kabla ya kuruka. Ndege ya Boieng chapa 737-500 ilipotea kwenye mawasiliano ya rada dakika nne baada ya kuruka.

Shirika hilo la ndege limesema kwenye taarifa yake kwamba safari ya ndege ilitarajiwa kutumia dakika 90 kutoka Jakarta hadi Pontianak, ambao ni mji mkuu wa jimbo la Kalimantan Magharibi kwenye kisiwa cha Borneo. Kulingana na mkurugenzi wake Jefferson Irwin Jauwena, ndege hiyo ilikuwa kwenye hali nzuri kabla ya kuruka.

Kulikuwa na jumla ya abiria 56 na wafanyakazi sita. Sumadi amesema meli kadhaa ikiwemo meli nne za kivita tayari zimesambazwa katika jitihada za kuisaka na operesheni ya uokozi tayari imeanza. Ripoti za vyombo vya habari zinasema wavuvi wameviona vipande kadhaa vya chuma vinavyoaminika kuwa sehemu ya ndege hiyo mchana wa Jumamosi kwenye maeneo ya visiwa.

Wanajeshi katika uwanja wa ndege wa Jakarta

Picha za kwenye televisheni zimeonyesha ndugu na marafiki wa jamaa za waliokuwemo kwenye ndege wakilia na kusali wakati wakisubiri kwenye viwanja vya ndege vya Jakarta na Pontianak. Indonesia nchi iliyo na visiwa vingi na yenye wakaazi zaidi ya milioni 260, imekuwa ikikabiliwa na ajali za ndege zinazotokana na usafiri wa ardhini, angani na baharini kwasababu ya kufurika kwa vivuko, ukuu wa miundombinu na utekelezwaji hafifu wa kanuni za usalama.

Mnamo mwaka 2018, ndege aina ya Boeing chapa 737 Max 8 inayoendeshwa na shirika la ndege la Lion Air, ilianguka baharini dakika chache baada ya kuruka kutoka Jakarta na kuwaua watu wote 189 waliokuwamo ndani. Ajali hiyo ndiyo ilikuwa mbaya katika majanga ya ndege ya Indonesia tangu mwaka 1997 wakati watu 234 walipouuwa kwenye ajali ya ndege ya Garuda karibu na Medan kwenye kisiwa cha Sumatra.

Mwaka 2014 ndege ya shirika la ndege la Air Asia iliyokuwa ikitoka mji wa Surabaya kuelekea Singapore ilianguka baharini na kuwaua watu 162


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages