NEWS

Tuesday 19 January 2021

Ni aina gani ya mazoezi yanayoweza kusaidia kuimarisha mifupa yako?

 

Unachofanya kwa mifupa yako wakati wa ujana kitakusaidia baadaye

Inafahamika vyema kwamba mazoezi ni mazuri kwa moyo, mapafu na ubongo. Lakini kuna sehemu moja ya miili yetu ambayo huwa inasahaulika nayo ni mifupa yetu.

Madaktari wa kipindi cha BBC cha 'Trust me- I'm a Doctor' waliamua kufanya uchunguzi kuhusiana na afya ya mifupa na hivi ndivyo wanavyoeleza.

Kadri tunavyozeeka, mifupa yetu inapungua uzito, jambo ambalo linaifanya kuwa dhaifu zaidi na kukabiliwa na uwezekano mkubwa wa kuvunjika

Baada ya miaka 35, tunapoteza takriban asilimia 0.5% ya ukubwa wa mifupa kila mwaka. Kupungua huku huongezeka zaidi hasa wanawake wanapofikia umri wa kutoweza kuzaa na kwa upande wa wanaume, baada ya miaka 50.

Ingawa madini ya calcium na vitamini D yanafahamika kuwa muhimu kwa afya ya mifupa yetu, tafiti zimeonesha kuwa mazoezi yanaweza kupunguza hali hii, au hata kuizuia kupungua kwa uzito wa mifupa na udhaifu wake kunakotokana na umri mkubwa.

Mazoezi yanaaminika kusaidia kuitunza mifupa yetu kwa kuifanya kuwa imara kwa kuiweka katika shinikizo la mazoezi.

Mazoezi ya mwili yanaaminiwa kuimarisha mifupa ya miili yetu

Inaaminiwa kuwa kila msukumo au shinikizo kwa mfupa wakati wa mazoezi hutuma taarifa kwenye seli za mifupa na hivyo kuifanya iwe imara tena.

Mifupa hupeleka taarifa kwa misuli ya mwili, ambayo kama imeimarika ipasavyo husaidia kuimarika kwa ujenzi wa mifupa.

Lakini ni aina ipi ya mazoezi ni muhimu kwa mifupa yako?

Ili kubaini hili tuliambatana na mtaalamu wa mifupa Dkt Karen Hind kuwafanyia uchunguzi wanariadha wakiwemo washindi wa medali za michezo ya Olympiki kama vile sarakasi, uendeshaji wa baiskeli na kriketi

Ni mazoezi mazuri lakini , lakini kama unafikiria kuhusu mifupa yako itabidi ufanye mazoezi mengine ya ziada.

Katika kuwachunguza wanariadha hawa tuliweza kubaini kuongezeka kwa uzito ambako kunaweza kutokana na aina fulani ya mazoezi ya mwili.

Hii ilitupa kiashiria cha aina gani za mazoezi zinazoweza kuinufaisha mifupa kwa kuiimarisha, miongoni mwa watu kwa ujumla na hivyo basi kusaidia kuzuia kuvunjika kwa mifupa siku zijazo.

Kukimbia ni moja ya mazoezi yanayoweza kuimarisha mifupa na misuli ya mwili wako

Baada ya uchunguzi wetu tuligundua kuwa ingawa sarakasi ilitarajiwa kuifanya mifupa kuwa imara zaidi, matokeo yetu kwa michezo kwa waendesha baiskeli na wacheza kriketi yalikuwa ya kushangaza.

Waendesha baiskeli walikuwa na mifupa mepesi katika uti wa mgongo na kiuno kuliko wastani, na wachezaji wa kriketi walikuwa na mifupa mizito zaidi miongoni mwa vikundi vya wanariadha waliofanyiwa vipimo.

Matokeo haya yanaonesha kuwa aina ya mazoezi au shughuli unazofanya vinaweza kuwa sababu ya kile tulichokishuhudia.

Wanasarakasi hupata athari chanya kutokana na kuruka na kutua, ambayo ni kuimarika kwa mifupa yao.

Uzito wa muendesha baiskeli hubebwa na baiskeli yake, kwahiyo huenda kusiwe na shinikizo la kutosha kwa mifupa yao ili kuiimarisha hususani mifupa ya uti wao wa mgongo.

Huku kuendesha baiskeli kukisaidia katika kuboresha afya yako ya mwili na afya ya moyo, vipimo vyetu vilionesha kuwa baiskeli sio nzuri sana inapokuja katika uimara wa mifupa yako.

Wacheza kriketi walitoa matokeo ya kustaajabisha - walionesha ukubwa zaidi wa mifupa katika vipimo vyetu.

Ingawa kuna mtizamo maarufu kwamba wacheza kriketi husimama wima kwa muda mwingi, matokeo yetu yalionesha kuwa muda wao mfupi wa kukimbia, kuruka na kuinama ni muhimu katika kuongeza uzito wa mifupa.

Ukubwa wa misuli pia ulionekana miongoni mwa wachezaji wa kriketi, hasa wanaume, na hili pia lilileta matokeo chanya katika mifupa yao.

Wataalamu wanashauri kuwa mazoezi ya misuli ni muhimu katika kuimarisha mifupa ya mwili hasa unapoongeza shinikizo kwa mifupa yako kwa njia ya mazoezi

Utafiti huu unatoa kiashiria kizuri cha ni aina gani ya mazoezi yanayoweza kuboresha afya ya mifupa yetu. Mazoezi yanayohusisha kuruka kidogo na kugeuza viungo vya mwili kama vile densi, yana uwezekano wa kuwa ya maana kwa mifupa yetu.

" Mazoezi bora kwa mifupa yako ", kwa mujibu wa chuo kikuu cha Harvard

Mwezi Mei, taarifa ya jarida la afya , kutoka kitengo cha chuo cha Harvard iliandika kuhusu "Mazoezi bora kwa mifupa yako " na kuelezea kwamba ni muhimu kuipatia changamoto ya mazoezi misuli yako kwa kuichosha kwa aina fulani ya mazoezi, kwa mfano, kwa kutumia vitu vizito, au kwa kutumia uzito mwili wako mwenyewe.

Michezo inayohusisha "kugeuka haraka kwa mwili na kuanza -na kusimama kwa mazoezi kwa haraka " husaidia kuimarisha mifupa.

"Mazoezi ya uvumilivu, ikiwa ni pamoja nay a kujenga misuli , hutegemea kupanuka na kusinyaa kwa misuli ambayo huvutwa kwenye mifupa na kuichochea kuongezeka uzito."

Kama kipindi cha BBC kilivyoonesha, wataalamu wa Havard pia walibaini kuwa " athari za mazoezi kwa ujumla ziliweza kuwa na atahari kwenye mifupa kuliko ukosefu wa mazoezi au kiwango cha chini cha mazoezi ."

Kwa mfano : " Unaporuka na kuanguka ardhini kwa kwa kila hatua unaokimbia , unaongeza mara dufu athari ya uzito wa mifupa."

Kutokana na uchunguzi huu orodha ya mazoezi yanayofaa katika kusaidia kuimarisha mifupa ni kama : upandaji wa milima, kupanda ngazi, kucheza tenisi, mpira wa pete na mpira wa kikapu, kwasababu michezo yote hii inahusisha kuruka hewani na kuanguka ardhini.

Jinsi ya kufanya mazoezi yanayoimarisha mifupa

Kasi ambayo unaitumia katika kufanya mazoezi huchangia katika uimarishwaji wa viungo vyako

Kasi ambayo unatumia katika kufanya mazoezi pia huchangia: " kukimbia au kufanya mazoezi ya haraka ya viungo vitaimarisha mifupa yako zaidi ya kutembea," inasema taarifa ya Havard.

Taarifa hiyo pia inashauri watu wasipuuze mazoezi ya kuboresha usawa wa mwili (stamina), kwasababu, ingawa hayasaidiikatika kuimarisha mifupa, husaidia kuzuia kuanguka.

Kwa umri wowote ulionao, kama una matatizo ya afya na unataka kuanza maozezi ya mwili ya kila wakati, ni muhimu kupata ushauri wa daktari kwanza ili uweze kuyafanya vema.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages