NEWS

Friday 22 January 2021

Waitara alaani mauaji ya wananchi Itiryo, atoa milioni 5/- kuchangia ujenzi kituo cha polisi

Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara akihutubia mkutano wa hadhara kijijini Itiryo, jana Januari 22, 2021.

 

MBUNGE wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara amelaani vikali mauaji ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika kata ya Itiryo na kusema lazima hatua za makusudi zichukuliwe kuimarisha usalama katani humo.

 

Waitara ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara katani hapo jana Januari 22, 2021 na ametoa Sh miloni tano kuchangia ujenzi wa kituo cha polisi katika eneo hilo.

Wananchi wakimsikiliza Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara (hayupo pichani) katika mkutano huo.

Tayari wananchi katika kijiji cha Itiryo wameshatenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho kinachotarajiwa kuwasaidia kuondokana na masaibu hayo.

 

Diwani wa Kata hiyo, Shadrack Marwa ndiye aliomba kituo hicho kupitia kwa mbunge huyo akisema usalama hafifu umekuwa kikwazo kikuu cha maendeleo ya wananchi katani humo.

Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara (kushoto mbele) akisalimiana na mkazi wa kata ya Itiryo kwa furaha siku ya mkutano huo.

Waitara ametumia nafasi hiyo pia kuwahimiza wananchi wa kata hiyo kuchapa kazi na kushirikiana na serikali katika kukomesha vitendo vya mauaji na uhalifu kwa ujumla.

 

(Habari na picha zote na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages