NEWS

Saturday 27 February 2021

Mbunge Ghati apiga jeki ujenzi kanisa la SDA Nkende

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Zephania Chomete akizungumza katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la SDA Nkende wilayani Tarime, leo.  

 

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Zephania Chomete, LEO Februari 27, 2021 amechanga Sh zaidi ya milioni mbili katika harambee ya ujenzi wa Kanisa la Waadventista Wasabato la Nkende wilayani Tarime.

Mbunge Ghati akiendelea kuzungumza katika harambee hiyo.

Katika harambee hiyo, Mbunge Ghati ameungwa mkono na viongozi mbalimbali wakiwemo Mbunge wa Tarime Mjini, Michael Kembaki aliyetoa Sh milioni 2.5 , Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Daniel Komote (sh 500,000)na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Samwel Kiboye maarufu kwa jina la Namba Tatu (saruji mifuko 50).


Pia vikundi vya kwaya kutoka maeneo mbalimbali wilayani Tarime vimejitokeza kushiriki harambee hiyo kwa kuchanga fedha taslimu.

Mbunge wa Tarime Mjini, Michael Kembaki (kushoto) akizungumza katika harambee hiyo. Kulia ni Mbunge Ghati.

Mbunge huyo kijana ameshukuru kualikwa kuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo ambapo pia amewaomba waumini wa kanisa hilo na wananchi kwa ujumla kuendelea kumwombea heri na kumuunga mkono Rais Dkt John Pombe Magufuli katika juhudi za kuwaletea Watanzania maendeleo ya kisekta.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Samwel Kiboye (Namba Tatu) akizungumza katika harambee hiyo.
 

Aidha, Mbunge Ghati ametumia nafasi hiyo pia kuwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko ikiwa ni pamoja na kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya.

 

(Habari na picha: Mara Online News)

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages