NEWS

Thursday 11 February 2021

TRA: Saruji kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki haitatozwa ushuru

Afisa Forodha Mwandamizi wa TRA, Godfrey Felician akizungumza na wafanyabiashara wa wilayani Rorya katika mkoa wa Mara, leo.


MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema mfanyabiashara yeyote anayeingiza saruji kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) haitatozwa ushuru wa forodha endapo bidhaa hiyo imekidhi kanuni za uasilia za Umoja Forodha wa Jumuiya hiyo (EAC Customs Union Rules of Origin, 2015).

 

Hata hivyo, Mamlaka hiyo imesema bidhaa hiyo italipiwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni asilimia 18 tu.

 

TRA imeyasema hayo kwenye semina ya kuelimisha wafanyabiashara kuhusu masuala ya ulipaji kodi na taratibu zake, iliyofanyika Shirati katika wilaya ya Rorya mkoani Mara, leo Februari 11, 2021.

Wafanyabiashara wa wilayani Rorya wakimsikiliza Afisa Forodha Mwandamizi wa TRA, Godfrey Felician katika semina hiyo.

 

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages