NEWS

Saturday 6 March 2021

Mbunge Ghati awabeba wanawake CCT, WAWATA Musoma Siku ya Maombi Duniani, awaahidi viti 100, mahema mawili

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Zephania Chomete (kushoto) akiteta jambo na baadhi ya wanachama wa umoja wa wanawake wa CCT na WAWATA Musoma wakati wa kilele cha Siku ya Maombi Kitaifa na Duniani mjini Musoma, jana. 

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Zephania Chomete, ameungana na umoja wa wanawake wa CCT na WAWATA Musoma kuadhimisha kilele cha Siku ya Maombi Kitaifa na Duniani na kuonesha shauku ya kuunga mkono juhudi zao za kujikwamua kiuchumi.

Mbunge Ghati akizungumza wakati maadhimisho hayo.
 

Akizungumza katika maadhimisho hayo mjini Musoma jana Machi 5, 2021, Mbunge Ghati ambaye alialikwa kuwa mgeni rasmi, ameupongeza umoja wa wanawake hao kwa kushiriki maombi hayo kitaifa na kidunia.

Wanachama wa umoja wa wanawake wa CCT na WAWATA Musoma wakishiriki maombi hayo.
 

Mbunge huyo kijana amewaeleza wanawake hao dhamira yake ya kuendelea kushirikiana nao katika kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla.

 

Kwa kuanzia, Mbunge huyo wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameahidi kuunga mkono umoja wanawake hao wa CCT na WAWATA Musoma kwa kuwapatia msaada wa viti 100 na mahema mawili.

Mbunge Ghati (katikati) akiwa amevishwa kitenge alichozawadiwa na umoja wa wanawake wa CCT na WAWATA Musoma.
 

“Tutaendelea kushirikiana katika kuinua uchumi wetu na wa Taifa, hivyo ninaahidi kuwaunga mkono kwa msaada wa viti 100 na mahema mawili kwa ajili ya mradi wenu wa kujiongezea kipato,” Mbunge Ghati amewambia wanawake hao.

 

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages