NEWS

Sunday, 28 March 2021

Rais Samia amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu TPA

Rais Samia Suluhu Hassan

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia, Samia Suluhu Hassan amesimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko kuanzia leo Jumapili Machi 28, 2021 kupisha uchunguzi dhidi ya ubadhirifu wa Sh bilioni 3.6 bandarini.

 

Rais Samia amefanya uamuzi huo leo Ikulu Dodoma, baada ya kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa mwaka 2019/2020.

Mhandisi Deusdedit Kakoko
 

“Waziri Mkuu aliunda kamati na wakafanya uchunguzi kidogo… hatua chache zilichukuliwa lakini imani yangu ni kwamba kama kuna ubadhirifu pale waliosimamishwa ni hawa wa chini huku, ninaomba mara moja nitoe agizo la kumsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa Bandari halafu uchunguzi uendelee,” amesema Rais Samia.

 

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages