NEWS

Friday 19 March 2021

Samia Suluhu Hassan rasmi Rais mpya wa Tanzania

 

Samia Suluhu Hassan akiapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo.

 

ALIYEKUWA Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, leo Ijumaa Machi 19, 2021 saa nne asubuhi, ameapishwa kuwa Rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Samia amekula kiapo hicho mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma katika Ikulu ya Magogoji jijini Dar es Salaam.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma (kulia) akimwapisha Samia Suluhu Hassan (kushoto) kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam.

 

Mara baada ya kula kiapo hicho, Rais Samia amekagua gwaride maalum la kijeshi.

 

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages