NEWS

Tuesday 20 April 2021

Hifadhi ya Serengeti yaendeleza juhudi za kuboresha uhusiano na vijiji jirani

Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Hobokela Richard (aliyesimama kulia) akielimisha wakazi wa kijiji cha Kitawasi wilayani Tarime umuhimu wa kutunza wanyamapori na mazingira.
 

HIFADHI ya Taifa ya Serengeti imeanza awamu nyingine ya kujenga na kuboresha uhusiano na ujirani mwema kati yake na wakazi wa vijiji vinavyopakana nayo katika wilaya ya Tarime mkoani Mara.

 

Katika juhudi hizo, hifadhi hiyo kupitia idara ya ujirani mwema imeanza kukutana na viongozi na wakazi wa vijiji hivyo kujadiliana kuhusu namna bora ya kushirikiana katika kutunza rasilimali za wanyamapori na mazingira.

 

“Mikutano hii ni sehemu ya jitihada zinazofanywa na TANAPA (Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania) katika kuboresha ujirani mwema ikiwa ni pamoja na kuwezesha wakazi wa vijiji hivi katika shughuli za kujipatia kipato kupitia vikundi,” Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Hobokela Richard amesema katika mkutano na wakazi wa kijiji cha Kitawasi, jana.

 

Kama ilivyofanyika katika mkutano na wakazi wa kijiji cha Kitawasi, Hobokela na wahifadhi wenzake kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wataendelea kutoa elimu ya uhifadhi wa rasilimali za wanyamapori, mazingira na faida zake, kujibu maswali na kupokea maoni ya wakazi wa vijiji vingine wilayani Tarime kwa siku kadhaa.

 

Mbali na kijiji cha Kitawasi, wahifadhi hao watafanya ziara kama hiyo katika vijiji vya Masurura, Masanga, Nyabilongo, Kenyamosabi, Karakatonga, Gibaso, Nyandage, Mangucha na Kegonga.

 

(Habari na picha: Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages