NEWS

Tuesday 6 April 2021

Mbunge Chege hakamatiki kwa utekelezaji ahadi Rorya

Mbunge wa Rorya, Jafari Chege akiwa kwenye katapila alilonunua na kulikabidhi kwa wananchi wa jimbo hilo.

MBUNGE wa Rorya mkoani Mara, Jafari Chege ameendelea kutekeleza ahadi zake kwa kishindo katika jimbo hilo na hivyo kuwa kielelezo bora cha utumishi wa kizalendo kwa wananchi.

 

Mojawapo ya ahadi zake kubwa alizotimiza kwa siku za karibuni ni ununuzi wa katapila (grader) kwa ajili ya kusaidia wana-Rorya kulima barabara ili kurahisisha shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi zinazohitaji miundombinu wezeshi ya barabara.

 

Mbunge Chege ametimiza ahadi hiyo Aprili 3, 2021 ambapo amekabidhi grader hilo kwa wananchi wa jimbo la Rorya, ikiwa ni miezi michache tu imepita baada ya kutimiza ahadi ya kuwanunulia wapigakura wake hao gari la kubeba wagonjwa (ambulance).

Mbuge Chege (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi siku aliyokabidhi katapila kwa wananchi wa jimbo la Rorya.

Kwa mujibu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano Ofisi ya Mbunge wa Rorya, grader hilo litaanza kutumika kwa utaratibu utakaowashirikisha madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, hasa kuhusu barabara zinazostahili kupewa kipaumbele katika matengenezo.

 

Barabara zote zitakazolimwa zitakabidhiwa kwa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) Wilaya ya Rorya kwa ajili ya kuzihudumia.

Mbunge Jafari Chege (mwenye shati na kofia ya njano kulia) akijinadi kwa wananchi wa Rorya katika moja ya mikutano yake ya kampeni za Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020.

(Habari: Mara Online News)

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages