NEWS

Thursday 8 April 2021

NHC, Rex Energy washusha msaada wa mabati 280 Rorya

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Charles Chacha (wa tatu kulia) akipokea msaada wa mabati 280 kutoka NHC na Kampuni Rex Energy. Wa pili kulia ni Kaimu Meneja wa NHC Mara, Eliaisa Keenja.
 

HALMASHAURI ya Wilaya ya Rorya leo Aprili 8, 2021 imepokea msaada wa mabati 280 yenye thamani ya shilingi milioni 8.5 kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Kampuni ya Rex Energy.

 

Kaimu Meneja wa NHC Mkoa wa Mara, Eliaisa Keenja amekabidhi mabati 160 yenye thamani ya shilingi milioni tano na Magori Wambura aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Rex Energy, Francis Khibisa, amekabidhi mabati 120 yenye thamani ya shilingi milioni 3.5.

WiKutoka kushoto ni Magori Wambura aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Rex Energy, Francis Khibisa, Diwani Samson Kagutu, Kaimu Meneja wa NHC Mara, Eliaisa Keenja, DED Rorya, Charles Chacha na viongozi wengine walioshiriki mapokezi ya msaada huo.
 

Wadau hao wa maendeleo wamesema wametoa msaada huo baada ya kuombwa na Mbunge wa Rorya, Jafari Chege kwa ajili ya kuezeka majengo mbalimbali ya shule za msingi na sekondari jimboni humo ili kuwezesha wanafunzi kupata vyumba vya kusomea bila msongamano.

 

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Charles Chacha amewashukuru wadau hao na kufafanua kuwa mabati hayo yatapelekwa kuenzeka vyumba vinne vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Nyang’ombe.

Mkurugenzi Chacha akielezea namna mabati hayo yatakavyotumika.

“Sasa tunakwenda kukamilisha majengo ya madarasa katika sekondari mpya ya Nyang’ombe ili isajiliwe na kupokea wanafunzi 105 tutakaowahamisha kutoka Shule ya Sekondari ya Nyamagaro,” amesema Chacha.

 

(Habari na picha zote: Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages