NEWS

Friday 9 April 2021

Watano hawa wanatakiwa kujisalimisha polisi haraka

Mwenyekiti wa KUU Mkoa wa Mara, Adam Kighoma Malima.
 

WAFANYABIASHARA watano wanatakiwa kujisalimisha haraka kwa Jeshi la Polisi mkoani Mara kwa ajili ya mahojiano kuhusu tuhuma za kuhamasisha watu kwenda kuiba mawe yenye dhahabu katika Mgodi wa Dhahabu wa North Mara.

 

Agizo hilo limetolewa na Kamati ya Ulinzi na Usalama (KUU) ya Mkoa wa Mara katika mkutano maalumu na waandishi wa habari mjini Musoma, jana Aprili 9, 2021.

 

Mwenyekiti wa KUU hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Kighoma Malima amewataja wafanyabiashara hao na maeneo wanakoishi yakiwa kwenye mabano kuwa ni Raphael Matiko Zakaria (Bweri mjini Musoma) na Keraha Yohana Chona (Nyamongo, Tarime).

 

Malima amewataja wengine kuwa ni Makenge Chacha Nyaisa (Nyamwaga, Tarime), Manasa Kazoya Philemon (Buswelu jijini Mwanza) na Nyagwisi Charles Marwa (Kemoge, Tarime).

 

Kiongozi huyo wa mkoa amefafanua kuwa wafanyabiashara hao wanatakiwa kujisalimisha haraka kwenye ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya kwa ajili ya mahojiano hayo.

 

(Habari: Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages