NEWS

Sunday 18 April 2021

Wapigaji wajichotea bilioni 2 za fidia Nyamongo

Mavurungutu ya noti za elfu kumi kumi za Kitanzania

MKUU wa Mkoa (RC) wa Mara, Adam Malima amesema uchunguzi umebaini kuwa watu wasiokuwa waamininifu wamechota shilingi bilioni mbili kiubadhirifu katika mpango wa fidia za mali za wananchi walioingizwa kwenye utaratibu wa kuhamishwa kupisha shughuli za Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, mwaka jana.

 

“Uchunguzi unaendelea, lakini kama bilioni mbili ni malipo ambayo hayakuendena na madai. Wananchi wa chini walifinywa, haki inaminywa,” RC Malima amewadokeza waandishi wa habari ofisini kwake, hivi karibuni.

 

Hata hivyo, mkuu huyo wa mkoa amesema tayari watuhumiwa 16 wametiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya kujipatia fedha za umma kiubadhirifu.

 

“Uchunguzi unaendelea na watu 16 wamefikishwa mahakamani,” amesema Malima bila kuwataja watuhumiwa hao.

Shughuli za usombaji mawe yenye dhahabu zikiendelea katika mgodi wa North Mara

Mpango wa fidia za mali mbalimbali za wananchi wanaotakiwa kuhama kupisha shughuli za uchimbaji madini katika eneo la Nyamongo ulihusisha shilingi bilioni 35 kupitia Benki ya CRDB.

 

RC Malima amesema Serikali haitavumilia watu wababe, au wenye nguvu ya kiuchumi wanaowakandamiza watu wa chini kwenye mpango wowote wa kulipa fidia katika eneo la mgodi wa Norh Mara.

 

(Habari: Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages