NEWS

Thursday, 25 December 2025

Waandishi Tarime washerekea Krismas kwa kutembelea wagonjwa


Mwenyekiti wa Reu Jacob Karoli (mbele) akiongoza waandishi wa umoja huo kukabidhi zawadi katika wodi ya wazazi
Na Godfrey Marwa,Tarime

Umoja wa kuwezesha Waandishi wa habari Wilaya ya Tarime, Reporters Empowerment Union (REU) wamesherekea Krismas kwa kutembelea Hospitali ya Halmashauri ya Mji Tarime na kukabidhi zawadi mbalimbali kwa wagonjwa.

Zoezi hilo la matendo ya huruma limefanyika leo Disemba 25, likiongozwa na Mwenyekiti wa Umoja huo Karoli Jacob,huku akiambatana na ViongoziWaandishi wenzake



Miongoni mwa zawadi hizo zilikuwa ni sabuni za kufulia na kuogea,mafuta ya kupaka na vinywaji aina juis kwa makundi yote yakiwemo wazazi,pamoja na wazee.

Aidha Umoja huo kupitia kwa Mwenyekiti wake, Karoli jacob ambaye pia ni mwandishi wa Habari wa Clouds Media mkoani Mara wameupongeza Uongozi wa Hospitali hiyo kwa huduma bora pamoja na wadau wa maendeleo wanaosapoti Umoja akiwemo Soya One Ltd, Abuu na Chichake.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages