NEWS

Monday 10 May 2021

TMDA yakabidhi taulo za kike za mamilioni kwa ajili ya wanafunzi mkoani SimiyuViongozi na wanafunzi wakifurahia makabidhiano ya taulo za kike mkoani Simiyu.

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) imetoa msaada wa taulo za kike zenye thamani ya Shilingi milioni sita kuunga mkono maandalizi ya kambi za kitaaluma mkoani Simiyu.

Akikabidhi taulo hizo juzi, Meneja wa TMDA Kanda ya Ziwa, Sofia Mziray amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili wasiangushe maono ya mkoa huo ya kushika namba moja kitaifa.


Msaada wa taulo za kike uliotolewa na TMDA.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka ameipongeza TMDA huku akipiga marufuku wanafunzi kujihusisha na uuzaji wa bidhaa mnadani, badala yake wahakikishe wanahudhuria masomo kikamilifu.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (katikati) na wanafunzi wakiendelea kufurahia msaada huo wa taulo za kike.

Ernest Hinju ni Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, amesema kambi za kitaaluma mkoani hapo zinatarajiwa kuanza Agosti 8, 2021 na tayari maandalizi yameanza.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa kike, Jackline Sonda ameishukuru TMDA na kuahidi kwamba watasoma kwa bidii kwani miongoni mwa sababu iliyokuwa ikiwafanya wasihudhurie masomo kikamilifu imepatiwa ufumbuzi.

(Habari na picha: Anita Balingilaki, Simiyu)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages