NEWS

Sunday 9 May 2021

Wananchi Bunda kufutwa jasho, machozi kwa milioni 209 mwezi huu



Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Damas Ndumbaro (kulia) akihutubia wananchi wa kijiji cha Kihumbu wilayani Bunda leo. Aliyekaa ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt Allan Kijazi.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt Damas Ndumbaro amesema Serikali imetenga Shilingi milioni 209 za kifuta jasho na machozi kwa wananchi wa wilayani Bunda mkoani Mara walioathiriwa kwa namna mbalimbali na wanyamapori wakiwemo tembo kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Dkt Ndumbaro amesema hayo leo Mei 9, 2021 alipokwenda kukagua mradi wa zahanati ya kijiji cha Kihumbu wilayani Bunda - ulioojengwa kwa mamilioni ya fedha zikiwemo Shilingi milioni 55 zilizotolewa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).

Sehemu ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Damas Ndumbaro (hayupo pichani) katika zahanati ya Kihumbu.

Amesema Shilingi milioni 209 za kifuta jasho na machozi zinazoelekezwa kwa wananchi hao zinatolewa na Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii.

“Milioni 209 ziko tayari na ndani ya wiki mbili zitafika Bunda,” amesema Waziri Ndumbaro na kubainisha kuwa hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya chama tawala - Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2020 - 2025.

(Habari na picha: Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages