Mbunge wa
Serengeti, Amsabi Mrimi akielekea kuingia bungeni jijini Dodoma, hivi karibuni. |
WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema Serikali itatoa Shilingi milioni 300 haraka iwezekanavyo kwa ajili ya kugharimia ukamilishaji wa ujenzi wa chujio la maji katika bwawa la Manchira lililopo Mugumu, Serengeti mkoani Mara.
Waziri Aweso amesema hayo bungeni jijini Dodoma hivi karibuni, wakati akijibu swali la Mbunge wa Serengeti, Amsabi Mrimi aliyetaka kujua ni lini mradi huo utakamilika ili kuwaondolea wananchi wa mji wa Mugumu na maeneo jirani tatizo la ukosefu wa maji safi.
Waziri
wa Maji, Jumaa Aweso akijibu swali la Mbunge Amsabi bungeni jijini Dodoma, hivi karibuni. |
Katika jibu lake, Waziri Aweso amefafanua kuwa ujenzi wa chujio hilo ni miongoni mwa miradi 177 ‘kichefuchefu’ ambayo imekuwa ikichafua jina la wizara hiyo.
Sehemu ya utekelezaji wa mradi wa bwawa la Manchira
“…wiki hii tunatoa pesa zaidi ya Shilingi milioni 300 ili kuhakikisha wananchi wa Mugumu wanaanza kupata huduma ya maji,” amesema Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Pangani mkoani Pwani.
Mbunge Amsabi akiwapungia wananchi (hawapo pichani) wakati akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maji jimboni kwake hivi karibuni
(Habari na Picha : Mara Online News)
No comments:
Post a Comment