NEWS

Saturday 29 May 2021

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa azindua Muongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mara



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (wa pili kutoka kushoto) akizindua kitabu maalum cha Muongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mara mjini Musoma, jana. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi na wa tatu kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Samwel Kiboye - Namba Tatu.

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amezindua rasmi Muongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mara katika hafla iliyohudhuriwa na mamia ya wadau mbalimbali kwenye ukumbi wa Mwembeni Complex mjini Musoma, jana Ijumaa Mei 28, 2021.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Mkuu Majaliwa ametoa wito kwa wadau kutoka ndani na nje ya mkoa wa Mara kujitokeza kwa wingi kuwekeza katika sekta mbalimbali mkoani humo akisema “Mara ni eneo muhimu na zuri kwa uwekezaji.”

Amesisitiza kwamba mkoa wa Mara una fursa nyingi za uwekezaji katika sekta za utalii, madini, kilimo, uvuvi, mifugo, viwanda, elimu, usafirishaji miongoni mwa nyingine na kwamba mazingira ya uwekezaji kwa wawekezaji ni rafiki kuanzia kwenye usalama hadi serikalini.

Awali, akizungumzia fursa ya uwekezaji kwenye sekta ya kilimo, Mkuu wa Mkoa (RC) wa Mara, Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi amesema mkoa huo una ikolojia nzuri inayostawisha mazao yote ya chakula na biashara.

Aidha, RC Gabriel amesisitiza kuwa amani na usalama vinavyoendelea kutamalaki katika mkoa wa Mara ni kivutio muhimu cha uwekezaji mkoani humo. “Amani na usalama vipo, usalama ni uchumi,” amesema.

RC Gabriel akielezea mkoa wa Mara ulivyojaaliwa kuwa na fursa lukuki za uwekezaji
 

Viongozi wengine ambao wamehudhuria hafla ya uzinduzi huo ni pamoja na Katibu Tawala Mkoa (RAS) wa Mara, Caroline Mtapula, Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Dkt Titus Kamani na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Mkoa wa Mara, Christopher Gachuma.

 

Aidha, wadau mbalimbali ikiwemo Benki ya CRDB na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wameshiriki na kupewa tuzo za kutambua mchango wao katika kufanikisha uzinduzi huo wa Muongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mara.

MaraOnlineNews-Uapdates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages