NEWS

Thursday 20 May 2021

WWF yakabidhi msaada wa pikipiki kuendeleza uhifadhi wa ikolojia ya Serengeti



Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu (kushoto) akimkabidhi Katibu wa Ikona WMA, Yusuph Manyanda pikipiki ambazo zilizotolewa na WWF kupitia mradi wa mabadiliko ya tabianchi unaofadhiliwa na Serikali ya Ujerumini.

SHIRIKA la Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF) limekabidhi msaada wa pikipiki sita za kisasa kwa Jumuiya za Hifadhi za Wamanyampori (WMAs) za Ikona na Makao ili kuendeleza juhudi za uhifadhi katika ikolojia ya Serengeti.

Msaada huo kutoka Serikali ya Ujerumani, umetolewa wakati ambapo mapato katika jumuiya hizo yameshuka kwa kiwango cha kutisha kutokana na janga la COVID-19.

Serikali ya Ujemurani imetoa msaada huo wa pikipiki maalumu kupitia mradi wa mabadiliko ya tabianchi unaotekelezwa nchini Tanzania na Shirika la WWF.

“Tunawezesha jumuiya za kijamii kukabiliana na uharibifu wa mazingira ikwemo uwindaji na katika ikolojia ya Serengeti,” Meneja wa mradi huo kutoka WWF,

Novati Kessy amesema juzi Jumatano katika hafla ya kukabidhi pikiiki hizo.

Kessy ameongeza “Katika ukanda huu wa Serengeti tumetoa pikiiki sita ambapo tatu ni kwa ajili ya Ikona WMA na tatu nyingine ni kwa ajili ya WMA ya Makao na lengo kuu ni uhifadhi.”

Meneja huyo amebainisha kuwa thamani ya kila pikipiki ni Shilingi milioni nane na elfu hamsini (8,050,000).


Meneja Mradi wa WWF, Novati Kesyy (kulia mwenye barokoa) akikabidhi msaada huo wa pikipiki rasmi kwa Mkuu wa Wilaya, Babu.

Akipokea msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurin Babu ameshukuru Shirka la WWF na wadau wake kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuhifahi ikolojia ya Serengeti.


Babu ametahadharisha watumshi wa jumuiya hizo kutotumia pikipiki hizo katika shughuli ambazo hazikukusudiwa kama vile bodaboda.

“Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, napenda kushukuru WWF kwa msaada huu. Hizi pikipiki ni mpya na lazima zitumike kustawisha uhifadhi endelevu,” amesema Babu.

Kuwa upande wake, Katibu wa Ikona WMA, Yusuph Manyanda amesema msaada huo wa pikiiki utasaidia kuimarisha doria katika eneo la WMA hiyo ambayo ni sehemu muhimu ya ikolojia ya Serengeti.

“Hizi pikipiki pia zitasaidia kupnguza gharama za uendeheshajia na hata kurudishha wanyamapori wanaovamia makazi ya wananchi,” amesema Manyanda.

Ikona WMA ipo katika eneo ambalo ni mapito ya wanyamapori yakiwemo makundi ya nyumbu wanaohama kila mwaka kutoka Hifadhi ya Taifa ya Seregeti kuelekeA nchini Kenya na kisha kurudi kazalia katika hifadhi hiyo bora Afrika.

(Imeandikwa na Mara Online News)

1 comment:

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages