NEWS

Monday 28 June 2021

Kwa kitendo hiki, Mhandisi Msafiri ameonesha uzalendo wa hali ya juu kwa serikali na nchi yakeNi Uzalendo wa hali ya juu. Ndivyo tunavyoweza kuelezea kitendo cha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Mhandisi Mtemi Msafiri (katikati) cha kujitokeza kushiriki kikamilifu katika Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru wilayani humo Jumatano iliyopita, licha ya kuachwa kwenye uteuzi wa wakuu wa wilaya, hivi karibuni. Miradi yote yenye thamani ya shilingi zaidi ya bilioni nne iliyokuwa imeandaliwa wilayani Tarime chini ya uongozi wa Mahandisi Msafiri, ilizinduliwa na Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021, Luteni Josephine Mwambashi, siku hiyo.


MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages